Shirika la habari AhlulBayt (a.s) ABNA: serikali ya umoja wa falme za kiarabu unawashikilia walimu wa Iran 9 waliokuwa wanafundisha shule za wairan wanaoishi nchini humo kwakilie kinacho daiwa kuwa ni kukosa visa ya nchini hiyo.
Polisi wa Emirates wamewakamata wairan hao na kuwapeleka msobemsobe katika kituo cha polisi, kitu ambacho kimeleta sura mbaya kwa walimu hao, huku taarifa zinaeleza kuwa balozi wa Iran nchi humo akishirikiana na viongozi wa wizara ya elimu ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran wanafanya juhudi za kuachiwa kwa walimu hao.
Sababu ya kukamatwa kwa walimu hao mpaka sasa haija fahamika, kwani walimu hao kwa muda mrefu mpaka sasa wako wakijishughulisha na masuala ya kufundisha nchini humo katika mashule ya wairan wanaoishi nchini humo kwa kutumia visa ya Dubai.
Mwisho wa Habari/290